Tuesday, October 30, 2012

RIPOTI YA MCT

RIPOTI YA TIMU MAALUM YA
UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA
JUKWAA LA WAHARIRI TANZANIA (TEF)
KUCHUNGUZA MAZINGIRA
YALIYOPELEKEA KUUAWA KWA
MWANDISHI WA HABARI
DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI CHA NYOLOLO, WILAYA
YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi
iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari
Tanzania (MCT) kwa kuzingatiaHadidu
za Rejea Timu hiyo ilizopewa na Baraza
la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
Imewasilishwa na:
John P. Mireny - Kiongozi wa Timu, MCT
Hawra Shamte - Mhariri wa Siasa, Gazeti la Mwananchi, TEF
Simon S. Berege - Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu Tumaini, Iringa
Yaliyomo
Orodha ya Ufupisho ...................................................................................... iii
1.0 Muhtasari wa Ripoti …………....................................……………… 1
2.0 Tamko la Tatizo …...........................................................…………… 2
3.0 Mamlaka ……………........................................……………………… 4
4.0 Hadidu za Rejea …………..................................……………………… 5
4.1 Lengo la Kuu ………...........................................…………………… 5
4.2 Malengo ya Mahsusi …………………...….................……………… 5
5.0 Muda wa kukamilisha jukumu ………………...............………….. 5
6.0 Methodolojia ……………………..........................…………………… 6
7.0 Matokeo ……................................................................……………… 7
7.1 Maelezo ya Awali ……...…………….......................……………….. 7
7.2 Eneo la matukio ya utulivu [A] …………………................……… 13
7.3 Eneo la umwagaji damu [B] …………..…….....………..................… 14
7.4 Matukio yasiyo ya kawaida katika eneo la umwagai damu [B] ..... 17
7.5 Mauaji ya Daudi Mwangosi ………….......................………………. 17
7.6 Taarifa rasmi zinazokinzana ………..................................………….. 19
7.7 Taarifa rasmi katika muktadha ………............................………….. 19
8.0 Iliyobaki yote ni historia ………………............................………….. 23
9.0 Shutuma na kulaaniwa kwa tukio kitaifa na kimataifa ................… 24
10.0 Hitimisho na Mapendekezo ……………………….........…………… 26
11.0 Picha za mauaji ya Daudi Mwangosi ………............……………… 30
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
ii
ORODHA YA UFUPISHO
CHADEMA – Chama cha DemokrasianaMaendeleo
CPJ – Kamati ya Kutetea Waandishi wa Habari
DCI - Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai
IPC - Klabu ya Waandishi ya Iringa
M4C - Harakati za Mabadiliko
MISA - Taasisi ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika
OC-CID - Mkuu wa Uchunguzi wa Makosa ya Uhalifu wa Wilaya
OCD - Mkuu wa Polisi Polisi wa Wilaya
RPC - Mkuu wa Polisi wa Mkoa
TEF - Jukwaa la Wahariri Tanzania
UNESCO - Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
iii
1.0 Muhtasari wa ripoti
Ripoti hii ni ya wa uchunguzi mazingira yaliyopelekea kuuawa kwa
Mwandishi wa Channel Ten Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi katika
kijiji cha Nyololo, wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa Septemba 2, 2012.
Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
kwa pamoja waliunda timu ya uhunguzi.
Mchakato wenyewe ulihusisha mbinu za uchunguzi za kiuandishi wa habari
ambazo si kama za uchunguzi wa kipolisi na wa kimahakama.
Methodolojia za uchunguzi zilijumuisha mahojiano, kutembelea maeneo
husika na uchambuzi mahsusi wa nyaraka kwa kuzingatia adidu za rejea
zilizopo. Waandishi wa Habari waliokuwepo Nyololo na ambao
hawakuwepo katika eneo la mauaji wametoa mchango muhimu.
Mashahidi walioshuhudia katika kijiji cha Nyololo, wakiwemo watoto
walikuwa vyanzo muhimu. Habari zilizochapishwa katika vyombo vya
habari kutokana taarifa rasmi kuhusu baa hilo pia zilichambuliwa kwa
umakini.
Uchambuzi mpana ulifanywa kuhusu hali ya mahusiano ya Uongozi wa
Mkoa wa Iringa( ikiwemo polisi) na wanahabari wa Iringa kabla ya mauaji
ya Mwangosi.Mahusiano yalikuwa si mazuri na ya shaka kati ya pande hizo
mbili tangu katika robo ya mwisho ya mwaka 2011.
Hii ilisaidia kupata picha pana ya tatizo pamoja na kuweza kufahamu kwa
undani tatizo lenyewe na kuweza kupanga mwelekeo wa uchunguzi
wenyewe na hatimaye kuwezesha timu kuweza kuunganisha mambo na
kuandaa ripoti hii.
Aina nyingine ya ushahidi uliosaidia kuimarisha ripoti hii ni pamoja na
video, picha mgando; maelezo kutoka katika mikutano na waandishi wa
habari iliyofanyika Iringa na taarifa za vyombo vya habari.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
1
Mpaka wakati ripoti hii inaandikwa, taarifa rasmi kuhusu mauaji ya David
Mwangosi zimekuwa zikitofautiana.
Kwa kifupi matokeo ya mambo yaliyopelekea mauaji ya Daudi Mwangosi
kwanza yanadhihirisha bila wasiwasi kwamba Polisi kwa makusudi
waliwaburuta waandishi waliotoka Iringa waliokuwa wakifuatlia habari za
shughuli za Chadema katika kijiji cha Nyololo. Zaidi ya hapo, Daudi
Mwangosi mwenyewe aliuliwa akiwa mikononi mwa polisi huku
wakiangaliwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Michael Kamuhanda.
Uamuzi huu unadhihirishwa na ushahidi uliokusanywa kwenye maeneo
pamoja na video na taarifa zingine za vyombo vya habari.
2.0 Tamko la Tatizo
Kuanzia Machi 2012 mahusiano ya kikazi kati ya waandishi wa habari wa
mkoa Iringa na viongozi wa utawala wa mkoa, ikiwemo jeshi la polisi,
haukuwa mzuri.
Katika mikutano yake mbalimbali ya kitaaluma, Klabu ya Waandishi Habari
ya Iringa (IPC) kutoka katika robo ya mwisho mwaka 2011, waandishi wa
habari wamekuwa wakilalamikia “kutotendewa sawa” na maofisa
wanapokuwa wakifuatilia na kuandika habari mkoani Iringa.
Kwa mfano , Novemba 2011, mwandishi Laurean Mkumbata anayeandikia
ITV alipigwa vibaya na kamera yake ikaharibiwa na aliyekuwa mkuu wa
polisi (OCD) wa wilaya ya Iringa , wakati mwandishi huyo alipokuwa
kazini.
Mkumbata alieleza mbele ya Timu ya Uchunguzi kwamba yeye na
waandishi wengine , akiwemo marehemu Daudi Mwangosi walikuwa
wakikusanya habari katika mpambano kati ya polisi na kundi moja la watu
mjini Iringa. Kundi hilo lilitaka kuchoma moto nyumba moja iliyodaiwa
kuwa na wachawi ambao uwepo wao ulikuwa ukiathiri eneo lote jirani.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
2
Hali iliyojitokeza ni kwamba ofisa yule wa polisi alitaka kuharibu kifaa cha
kazi cha mwandishi ili kuzuia upelekaji wa habari kuhusu mpambano wa
wananchi wenye hasira na polisi.
Wakati polisi walikuwa wakiwadhibiti watu hao kwa kutumia mabomu ya
machozi na kufyatua risasi za moto hewani kuwatisha na kuwaondoa watu
hao kutoka eneo la tukio, OCD Semunyu alimshika mwandishi huyo na
kumnyang’anya kamera yake ambayo aliipiga chini mara tatu, na hivyo
kuiharibu kabisa.
Pamoja na hayo, Mkumbata alishikiliwa kwa muda alipokwenda kutoa
taarifa kuhusu tukio hilo katika makao ya polisi ya mkoa. Baada ya hapo
jitihada za kuficha ukweli zikaanza.
Hata hivyo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa (RPC),
Evarist Mangala aliingilia kati na kumwamuru ofisa aliyehusika, Semunyu,
kulipa kamera iliyovunjwa. Ofisa huyo alitekeleza amri hiyo na Mkumbata
alipata kamera yake. Ofisa huyo alilipa kutoka mfukoni mwake.
Mkumbata anaamini kwamba ofisa yule wa polisi aliipiga chini kamera yake
mara tatu kuhakikisha inaharibika kabisa na hakuna kinachopatikana, hatua
iliyolenga kuhakikisha mwandishi huyo hawezi kutangaza taarifa za tukio
kwa wakati.
Tangu wakati huo hali ya kutiliana shaka imekua katika mahusiano ya
wanahabari wa Iringa na Polisi. Mahusiano na viongozi wengine wa mkoa
nayo hayajakuwa mazuri tangu kipindi hicho cha robo ya mwisho ya 2011.
Frank Leonard, Katibu wa IPC anakumbuka kuwa mwishoni mwa
Februari 2012, waandishi saba waliteuliwa na IPC kuandika habari ya ziara
ya Makamu wa Rais mkoani Iringa, lakini walilazimika kulala ndani ya basi
walilosafiria kwa kuwa maofisa wahusika wa mkoa walidaiwa kupuuza
kuwapatia hoteli ya kulala.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
3
Tukio hilo liliudhi uongozi wa IPC ambao uliandaa maandamano ya amani
kulalamikia unyanyasi wa waaandishi wa habari unofanywa na viongozi
wa mkoa.
Hatua hiyo, kwa mujibu wa Katibu huyo ililenga kuwasilisha kwa viongozi
wa mkoa msimamo kwamba “Wanachama wa IPC hawaegemei chama
chochote cha siasa, bali ni wanataaluma na wanaosimamia uandishi habari
unaozingatia maslahi ya umma”.
Machi 6, 2012, mamlaka ya polisi ya mkoa uliidhinisha ombi la IPC
kuandamana kupinga kuendelea mahusiano yasiyo mazuri kati ya
waandishi wa habari na uongozi wa mkoa.
Katibu wa IPC anakiri kwamba mahusiano kati ya pande hizo mbili
yaliboreka baada ya maandamano hayo ambapo aliyekuwa Kamanda wa
Polisi wa Mkoa aliahidi kushughulikia tofauti zilizopo na kuhakikisha
kunakuwa na maelewano.
Kubadilika kwa mambo ghafla na kufikia mauaji ya Daudi Mwangosi hapo
Septemba 2, 2012, wakati a akikusanya habari za shughuli za kisiasa za
Chadema katika wilaya ya Mufindi , katika kijiji cha Nyololo mikononi
mwa polisi wanaotuhumiwa kwa mauaji inastusha na ni jambo lisilo la
kutegemewa kwa Frank Leaonard. Marehemu Daudi Mwangosi alikuwa
Mwenyekiti wa IPC.
3.0 Mamlaka
Mamlaka ya uchunguzi huu inatokana na katiba ya Baraza la Habari
Tanzania (MCT), kifungu 3 (e), kinachoelezea malengo ya Baraza kuwa ni:
Kuwa na rejista ya matukio yanayoweza kukwaza upatikananji wa habari za manufaa
kwa umma na muhimu, na kuchunguza tabia za watu, mashirika na vyombo vya
serikali kwa ngazi zote dhidi ya vyombo vya habari, na kutangaza matokeo ya
uchunguzi huo.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
4
3.1 Lengo
Lengo la uchunguzi huo ni kuweka rekodi sawa ya mazingira yaliyopelekea
kuuawa kwa mwandishi wa Channel Ten na Mwenyekiti wa IPC, David
Mwangosi , Septemba 2, 2012 katika kijiji cha Nyololo , wilaya ya Mufindi,
mkoa wa Iringa .
Uchunguzi huo ni huru na sio kama wa kipolisi au wa kimahakama lakini ni
jitihada za dhati za kuweka kumbumbuku ya hali ya mambo kuhusu kifo
cha kwanza cha mwandishi wa Tanzania akiwa kazini.
4.0 Adidu za Rejea
Timu ya uchunguzi iliongozwa na Adidu za Rejea zifuatazo:
4.1 Lengo Kuu
Kuchunguza hali iliyopelekea kuuawa kwa David Mwangosi.
4.2 Malengo mahsusi
Kuchunguza chanzo cha kuwepo uhusiano usio mzuri kati ya IPC na
uongozi wa kiutawala wa Iringa .
Kuwahoji wanakijiji wa Nyololo kuhusu hali halisi iliyosababisha
mapambano kati ya polisi/ Chadema/ waandishi wa habari.
Kukusanya maelezo stahili kutoka kwa wananchi, IPC na mashuhuda
waandishi waliokuwepo kwenye eneo la ghasia.
Kuchambua kwa uhuru ripoti za vyombo vya habari, ripoti rasmi na za polisi
na madai kuhusu tukio hilo.
5.0 Muda wa kukamilisha jukumu
Kazi hiyo ilichukua siku nane (8) kuanzia Septemba 5, 2012 na kumalizika
Septemba 12, 2012.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
5
6.0 Methodolojia
Timu ilianza uchunguzi kama ifuatavyo:
Kwanza kabisa, hati na taarifa za magazeti kuhusiana na uchunguzi huo
zilipitiwa ili kupata msingi wa suala hilo. Hii inajumuisha mamlaka ya
kikatiba ya MCT kufanya uchunguzi kama huo.
Pili, Timu hiyo imechunguza kwa karibu jinsi vyombo vya habari
vilivyotangaza zikiwemo picha mgando, na video kuhusu kuuawa kwa
Daudi Mwangosi hapo Septemba 2, 2012, na taarifa za awali za polisi dhidi
ya mambo yaliyogunduliwa na wachunguzi katika uchunguzi wao. Taarifa
zote zilizoripotiwa na polisi na Waziri mwenye dhamana kuhusu mauaji ya
mwandishi kabla yataarifa ya kuundwa kwa kamati maalum ya uchunguzi
ya Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Emmanuel Nchimbi Septemba 4, 2012
yanachambuliwa kwa kina.
Hatimaye, uchunguzi katika eneo. Hii ilihusisha kusafiri kwenda Iringa na
kufanya mahojiano na watu walioteuliwa na wanahabari katika kijiji cha
Nyololo waliokuwepo siku Mwangosi. Utaratibu wa mahojiano ya
mtiririko kutokana na majibu ulitumiwa na wachunguzi kwa watu
mbalimbali.
Utaratibu mkuu ulikuwa ni mazungumzo ya bayana kati ya wachunguzi na
watu mbalimbali wakiwemo baadhi ya wanakijiji wa Nyololo. Mbinu za
kiuchunguzi za uandishi wa habari zilitumika kufanikisha lengo la jukumu
hilo.Matokeo yake, mchakato huo uliwezesha kupatikana ukweli
uliowezesha kukamilisha ripoti.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
6
7.0 Matokeo
7.1 Maelezo ya awali
Hapo Septemba 2, 2012, mikutano miwili tofauti ya waandishi wa habari
iliyosheheni ilifanyika katika Manispaa ya Iringa kwa nyakati tofauti siku
hiyo. Mkutano wa kwanza uliitishwa na kuhutubiwa na Kamanda wa Polisi
wa Mkoa wa Iringa (RPC), Michael Kamuhanda katika ofisi yake
asubuhi.
Mada ya mkutano huo ni uamuzi wa polisi kuzuia mikutano ya kisiasa
iliyopangwa na chama cha upinzani cha Chadema katika mkoa wa Iringa
iliyolenga kutelekeza kampeni za chama hicho za Kuleta Mabadiliko nchi
nzima.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa alitahadharisha kuwa sensa ya watu na
makazi ambayo awali ilikuwa ilipangwa kufanyika Agosti 26 – Septemba
1, 2012, imeongezewa muda na serikali hadi Septemba 8, 2012, na
mikusanyiko ya kijamii na mikutano ya kisiasa imesimamisha mpaka zoezi
hilo likamilike.
Waandishi wa habari waliokuwepo kwenye mkutano huo wanakiri kwamba
katika mkutano huo marehemu Daudi Mwangosi alikuwa ni ripota pekee
aliyemuuliza RPC “maswali magumu” kiasi cha kumkera kiongozi huyo
wa polisi.
Mojawapo ya maswali yaliyoulizwa na Mwangosi ni ufafanuzi sahihi wa
nini hasa ni “ mkutano wa ndani wa chama” kulingana na madai ya maofisa
wa Chadema kwamba chama hicho hakipangi kufanya mikutano ya
hadhara na maandamano ya kisiasa bali ni kufungua matawi mkoani Iringa
bila kufanya mikutano.
Katibu wa IPC anakumbuka swali moja la Mwangosi kwenye mkutano huo
ambalo lilimuudhi RPC. Aliuliza: kwanini chama tawala cha CCM kiko
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
7
huru kufanya mikutano ya kisiasa wakati chama cha upinzani kama
Chadema kinawekewa vikwazo na polisi kila wakati.
Wakati marehemu Mwangosi akisisitiza ufafanuzi zaidi kutoka kwa Mkuu
huyo wa polisi wa mkoa, RPC alisisitiza : “ Hii ni amri na polisi hairuhusu
maswali zaidi kuhusu suala hili”.
Na taarifa kutoka kwa RPC imewakumbusha wazi wanasisasa, vyama vya
siasa na wananchi kwa jumla kwamba “mikutano ya vyama vya kisiasa
imezuiliwa kutokana na kuendelea kwa sensa ya watu na makazi kwa siku
saba zaidi kuanzia Septemba 2, 2012.
Mara baada ya mkutano na RPC baadhi ya maofisa wa polisi walionyesha
kuwa mambo hayatakuwa sawa katika kijiji cha Nyololo village
Waandishi wengine wa Iringa, Clement Sanga anayeandikia magazeti ya
Mwananchi Communications Ltd na Oliver Motto, mwandishi wa
kujitegemea wa gazeti la Mtanzania, Star TV na Radio Free Africa walisema
haya :
“Baada ya mkutano huo na waandishi , wakati wanahabari wakitoka
kwenye ofisi za mkoa za Polisi, baadhi ya polisi walisikika bila wao kuwa
wakiwaonya wasiende Nyololo kwa ajili ya kukusanya habari za shughuli za
siasa za Chadema kutokana na kuwa na uwezekano wa hatari”.
Mkutano wa pili wa waandishi uliitishwa mchana na Chadema na
ukahutubiwa na Katibu Mkuu na Dk.Wilbroad Slaa na kamanda wa
Kampeni ya Mabadiliko ya chama hicho Benson Kigaila.
Katika mkutano huo , Chadema ilichachamaa na kutetea kampeni zake za
mabadiliko na kushutumu polisi kwa kufanya njama za kuzima kamepni
hizo. Chadema ilihoji kwanini polisi inabagua vyama vya upinzani wakati
wakipendelea chama tawala CCM kwa madai ya kusimamia sheria.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
8
Licha ya kuwepo amri ya polisi ya kuzuia mikutano yote ya siasa mpaka
zoezi la sensa ya watu na makazi lililoongezewa muda limalizike , Chadema
ilidai kwenye mkutano huo kwamba kampeni za uchaguzi za CCM katika
uchaguzi mdogo ziliruhusiwa kufanyika katika jimbo la Bububu , Zanzibar.
Kampeni za uchaguzi mdogo wa Bububu zilizinduliwa Jumapili Septemba
2, 2012 na Makamu wa Rais wa serikali ya Muungano, Dk. Mohammed
Gharib Bilal.
Hivyo kwa ufupi, Chadema iliamua kuendelea na kampeni zake mkoani
Iringa , ikiwemo kufungua matawi ya chama katika kijiji cha Nyololo,
wilaya ya Mufindi Jumapili Septemba 2, 2012, lakini bila kufanya mikutano
ya hadhara.
Hatimaye maofisa walishikilia msimamo wao na kuendelea kufufungua
matawi ya chama Nyololo. Kamanda wa Polisi wa Mkoa Iringa, RPC
Michael Kamuhanda, alipanga askari wake kwenye magari ya wazi
kufuatilia msafara wa maofisa wa Chadema. Pande hizo mbili zilikutana
kwenye kijiji cha Nyololo.
Viongozi wa Chadema walipanga kufungua matawi mawili katika kijiji cha
Nyololo village, kiasi cha kilomita 500 (315 maili) magharibi mwa Dar es
Salaam, na mwendo wa saa tatu kwa gari kutoka Manispaa ya Iringa.
Matawi hayo yako umbali wa kilomita tatu kutoka kila moja
yakitenganishwa na barabara kuu ya Dar es Salaam -Tunduma.
Mchoro uliopo ukurasa wa 16 unaonyesha hali halisi ilivyokuwa, kama
ilivyoelezwa na mashuhuda waliokuwepo na kuboreshwa na wachuguzi.
Kwa lengo la kuonyesha , maeneo mawili yamewekewa alama tofauti ya A
ikimaanisha “eneo tulivu” na B ikimaanisha “eneo la umwagaji damu”.
Katika eneo la [A], ambapo utulivu ulikuwepo na ulizingatiwa na polisi
katika maamuzi na matendo yao ambapo vurugu na umwagaji damu
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
9
uliepukwa. Eneo lingine ni [B], ambapo polisi ilitumia, nguvu zaidi na
kupelekea mauaji ya Daudi Mwangosi na kujeruhi waandishi wengine
kadhaa wa Iringa na makada wa Chadema.
7.2 Eneo la matukio ya utulivu [A]
Hapa ni sehemu ya kwanza lilipo tawi la Chadema kusini mashariki mwa
barabara ya changarawe inayopita kijiji cha Nyololo, kutoka barabara kuu
ya Dar-Tunduma.
Mashuhuda (waandishi na wanakijiji) wal;isema kuwa baada ua kuwasili
kwenye eneo la tawi, maofisa wa Chadema na wanachama walishuka
kutoka kwenye magari wakiwa tayari kuanza shughuli. Ukanda wa njano
uliwekwa kuzunguka ofisi ya Chadema kuzuia watu kukusanyika katika
jingo la ofisi hiyo.
Mara baada ya Chadema kuanza mkutano wao wa ndani kikundi cha askari
wa kikosi cha kuzuia fufo (FFU) kilifika eneo hilo na kujipanga kwa muundo
wa kijeshi wa V. Kikosi hicho kilikua chini ya uongozi wa Ofisa wa kudhibiti
uhalifu wa mkoa (RCO) SSP Nyigesa Wankyo.
Kamanda wa kikundi cha FFU OC Florent Mnunka anaamuru polisi wainue
bendera nyekundu yenye maandishi ya kuwataka watu waliokusanyika
kutawanyika ama vinginevyo watatumia nguvu. Kamanda huyo anatangaza
“Watu wote mliokusanyika hapa, mnaamriwa na Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania mtawanyike mara moja na kwa amani, vinginevyo tutatumia
nguvu ” anarudia maneno hayo . Baada ya kurudia amri hiyo mara tatu,
OC-CID anaamuru polisi kusogea karibu na ofisi ya Chadema.
Wakati wakisogelea eneo hilo la Utulivu [A] , Kamanda wa kampeni ya
mabadiliko ya Chadema Benson Kigaila na viongozi wengine walitoka nje
ya ofisi hiyo na kumuomba kamanda wa FFU kuzuia askari wake kutumia
nguvu bila sababu kwa kuwa haikupanga kufanya mkutano wa hadhara
wa kisiasa.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
10
Viongozi wengine waliokuwa na Kigaila walikuwa ni Alfred Lwakatare
na Naibu Katubu Mkuu wa Chadema Zanzibar , Said Issa Mohamed.
Pande hizo mbili zilipingana kwa muda kuhusu maana sahihi ya“ mkutano
wa ndani wa chama” na kama maana yake ni tofauti na mikutano iliyozuiwa
na polisi .
Ushahidi wa picha za video uliopatikana na waandishi wa habari wengi
unadhihirisha na kuonyesha mvutano kati ya polisi na Chadema katika
eneo tulivu[A] kama ifuatavyo:
Benson Kigaila: “ Sisi tuko katika ofisi ya tawi letu, tunajua sheria , hili ni
tawi la Chadema”.
Kamanda wa FFU : “Tunawaonyeni nyingi, tafadhali, fanyeni mkutano
wenu ndani ya ofisi”
Benson Kigaila: “Hatuendi kokote ”
Kamanda wa FFU: “Ingieni ndani”
Ghafla RCO akaingilia na kushauri viongozi wa Chadema kuwaambia
wananchama wao waingie ndani ya ofisi yao..Wanachama walikubali lakini
wote wasingeweza kutosha kwa sababu ofisi yenyewe ni ndogo. .
RCO akasisitiza: “Huu ni mkutano usioruhusiwa, tafadhali ingieni ndani”
Mwenyekiti wa Taifa wa vijana wa Chadema (Bavita), John Heche akajibu :
“Tatizo ni nini? Kama mmetumwa kuua, fyatueni risasi na muue…sisi
tutakaa hapa.”
Kijana mmoja wa Chadema anasikika katika video akiwaambia polisi ;
“Jana makada wa CCM walirejesha fomu za uchaguzi wa chama chao kwa
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
11
maandamano na sherehe … sisi hatuko tayari kuondoka ”.
John Heche anabishana na polisi akisema : “Mfahamu sheria zenu kabla ya
kufanya kazi yenu”
Mwishowe, maelewano yalifikiwa kati ya RCO na maofisa wa Chadema ,
na kamanda anaamuru maofisa wake kutotumia nguvu dhidi ya watu
waliokusanyika kwenye ofisi ile.
Ofisa mmoja wa Polisi analalamika , “Wanatupotezea muda wetu ….aaah
wanachukua muda wetu”.
Ofisa huyo inaelekea alikuwa akilalamikia amri ya mwisho iliyotolewa na
mkuu wake, RCO, ikikitaka kikisi hicho kuacha kutumia nguvu, ikiwa
inakiuka amri awa awali.
Waandishi dhidi ya RPC Kamuhanda
Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Michael Kamuhanda anawasili kwenye eneo
la utulivu [A] dakika chake baada ya RCO, maofisa wa FFU na wa
Chadema kufikia muafaka na kukubaliana kuhusu maana ya “mkutano
wa ndani”. Waandishi waliokuwepo eneo hilo walimpokea kwa maswali
kadhaa kuhusu tofauti za polisi na Chadema. Marehemu Daudi Mwangosi
akiwa mmoja wa waandishi hao waliomkabili RPC.
Mwangosi alimuuliza RPC: “Watu hawa wako katika eneo la ofisi yao, kuna
tatizo lolote linalotokana na shughuli wanazokusudia kufanya?”
RPC anamjibu Mwangosi “Nimeshakuambia usiwe mbishi. Nilichokuambia
ni kwamba nimezuia mikutano yote ya kisiasa…Lakini usije na mambo yale
yale asubuhi, jioni na mchana, na jua linapozama…kuna umuhimu gani
kutuuliza sisi tupo hapa kufanya nini?”.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
12
Mwandishi mwingine (Jina lake halikutapitkana ) “Nafikiri wewe ndiye
mbishi (RPC)”
RPC “Nilichozuia ni mikutano ya hadhara ya kisiasa, lakini shughuli zote
za ndani zinaruhusiwa kuendelea…hadi sasa hakuna tatizo”
RPC anaendelea: “Tumefanikiwa kuzuia mikutano na ghasia… kama
wanataka kufanya mikutano ya ndani wanaweza kuendelea.”
Mwangosi “…kama wanavyofanya sasa …..…”
RPC anajibu, “Kama walivyofanya tangu juzi ”
Baada ya kubadilishana maneno zaidi RPC anasema: “Tunawataka
viongozi, hatutashughulika na watu waliokusanyika hapa. Lengo letu ni
kushughulikia walioitisha mkutano… wao ndio chanzo cha kila kitu, na
wanavunja amri rasmi”. Tunaogopa kuwajeruhi watu bila sababu, hivyo
tutashughulika na viongozi ambao ni kundi dogo na ni rahisi
kulishughulikia” anasema RPC na kuamuru “Sasa hakuna mkutano, huu
(mkusanyiko) unaofanyika nje.”
Mwangosi anaingilia: “ Huu ni mkutano ?
RPC anaamuru mkusanyiko kuendelea na mkutano wao ndani; “Ingia
ndani”
Mwandishi ( anayetambulika kwa kubeba kamera na akiwa katika kundi la
waandishi): “Inakuwaje kama chumba ni kidogo kutosha watu wote?”
RPC: “Tutawakamata ninyi viongozi kama mtaendelea ”
Sauti ya mtu anayedhaniwa kuwa kiongozi wa Chadema inasema:
“Tutaendelea kuwapo hapa .”
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
13
RPC: “Ndiyo na ninyi mko wachache, tunawamudu ”
Mtu huyo anajibu : “Aah! Hamna tatizo… ni miaka mingapi Mandela alikaa
gerezani ”?
RPC anajibu , “ Hata miaka 30, lakini umemtaja Mandela, wewe Mandela?”
Wakati waandishi wakimhoji RPC, maofisa wa Chadema waliendelea na
mkutano wao na kuumaliza kwa amani. Chadema walimaliza shughuli yao
na wanahabari wakafanya kazi yao hapa bila kunyanyaswa.
Baaada ya hapo makada wa Chadema walipanda basi lao kwenda kaskazini
magharibi kwenye ofisi nyingine. Katika eneo hili la utulivu. [A],mabomu ya
machozi hayakulipuliwa wala risasi hazikupigwa kuwatisha watu. Pia
hakuna mtu aliyeuawa.
7.3 Eneo la umwagaji damu [B]
Mara baada ya maofisa wa Chadema kumaliza ufunguzi wa tawi katika eneo
la utulivu [A], walikwenda kukamilisha shughuli katika eneo la umwagaji
damu [B].
Inachukua chini ya dakika 20 kutembea kufika katika ofisi ya pili ya
Chadema. wakati maofisa wa chama wakielekea katika eneo hilo, polisi
waliwafuata kwa karibu. Waandishi wa habari pia waliwafuatilia ili
kukusanya habari za shughuli hiyo.
Lakini kitu kimoja kibaya kilitokea hata kabla ya askari wote wa FFU
kufika katika eneo la Umwagaji damu [B].
Mashuhuda wanaeleza kuwa RPC alimwita RCO na kumuonya wazi
kuhusu “ kushughulikia kwa amani’ masuala ya Chadema katika eneo la
awali la utulivu [A].
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
14
Inaelekea RCO alijitoa kuelekea eneo la umwagaji damu [B], na hivyo
usimamizi wa utoaji maamuzi katika Eneo la Umwagaji damu [B] ulibakia
kwa mkuu wake ambaye ni RPC Michael Kamuhanda.
Mabishano na waandishi wa habari kama yaliyotokea katika eneo la la
awali yaliibuka tena.
Hapa makada wa Chadema walikusanyika nje ya ofisi yao wakiimba t
“Wamezoea kuua , wamezoea kuua”. Inaelekea wimbo huo uliwaudhi polisi.
Vurugu zikaanza pale RPC alipoamuru kukamatwa kwa viongozi wa
Chadema waliokuwepo, kwa mujibu wa watu walioshughudia. Kufuataia
amri hiyo ya RPC kulingana na mashuhuda , polisi kwanza waliingia kwa
nguvu katika ofisi ya Chadema, wakipiga mabomu ya machozi na
kuaamuru viongozi hao wajisalimishe.
Baada ya polisi kutumia nguvu, kiongozi wa kampenu za mabadiliko wa
Chadema mkoani Iringa, Benson Kigaila , aliwaomba wafuasi wachache wa
chama hicho na viongozi waliokuwepo kujisalimisha kwa kuketi na kuinua
mikono yao juu”.
Waandishi wawili waliohojiwa, Clement Sanga wa Mwananchi
Communications Ltd na Oliver Motto, mwandishi wa kujitegemea wa
Mtanzania, Star TV na Radio Free Africa walishuhudia ghasia hizo katika
kijiji cha Nyololo village, wakati wakiwa wamekimbilia sehemu ya
barabarani, hatua chache kutoka eneo hilo la umwagaji damu B.
Waandishi hao walisema kuwa wakati makada wa Chadema walitii
maagizo ya viongozi wao ya kuketi na kuinua mikono yao juu, polisi
walifyatua risasi na n a mabomu ya machozi, na kuwapiga makada hao na
waandishi kwa virungu.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
15

16
7.4 Matukio yasiyo ya kawaida katika Eneo la Umwagaji Damu (B)
Jambo moja la kushangaza katika eneo la umwagaji damu B ni kuwepo
kwa raia wachache (makada wa Chadema na waandishi kwa pamoja),
wakiwa wamezidiwa kabisa na idadi ya polisi. Maelezo ya mashuhuda,
picha mgando na video zinadhihirisha hii bila shaka yoyote.
Wanakijiji wa Nyololo waliohojiwa walisema kwamba Jumamosi
Septemba 1, 2012 watu wanaoaminika kuwa ni askari kanzu walifika eneo
hilo na kuwaonya wakazi wake kuhusu ya hatari inayowza kutokea kama
wakihudhuria shughuli za ufgunguzi wa matawi ya Chadema. Walidai
kuwa walishauriwa pia kuondoka katika maeneo yao wakati wa saa za
mchana Jumapili Septemba 2, 2012 wakati ambao Chadema imepanga
kuendesha shughuli zake.
Mkakati wa kutisha ulifanikiwa kwa sababu watu wazima wakazi wa
Nyololo waliohojiwa baadaye walisema hawajui kuhusu vurugu za polisi
na Chadema kwa sababu walitelekeza ushauri wa kuondoka katika maeneo
hayo.
Mwanamke mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema:: “Nimejua
kuhusu ghasia hizo na kifo cha mwandishi wa habari kijijini kwetu baada
ya kurejea nyumbani jioni.” Kutokana na uvumi wa vitisho uliosambazwa
Jumamosi Septemba 1st, 2012, nilipanga kumtembelea jamaa yangu aliye
mbali kama njia ya kuepuka”.
7.5 Mauaji ya David Mwangosi
Baada ya kumaliza ukusanyaji wa habari kwa amani katika enelo la utulivu
[A], waandishi wa habari walikwenda katika eneo ambalo liligeuka kuwa
mtego wa kifo Eneo la Umwagaji damu [B] kutoka mwelekeo wa kusini
mashariki kupita barabara kuu ya Dar-Tunduma kumalizia kazia yao.
Alipoangalia nyuma , Daudi Mwangosi aliona kikundi cha polisi
wakimpiga mwandishi mkuu wa gazeti la Nipashe, wa Iringa, Godfrey
Mushi (32).
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
17
Mwandisi huyo alipigwa mpaka akapoteza fahamu na akapata fahamu
akiwa kwenye kituo cha polisi cha Mafinga. Kamera yake, daftari lake na
kalamu havikupatiakana.
Wakati mwandishi Godfrey Mushi akiwa bado anapigwa na polisi,
marehemu Mwangosi aliwakimbilia akiwaomba waache kumdhuru zaidi
Mushi kwa kuwa alikuwa mwandishi tu.
Polisi hawakumsikiliza. Badala yake wakamburuta mwandishi huyo ambaye
tayari alikuwa amepoteza fahamu na kumweka kwenye gari lao na
wakamgeukiwa Daudi Mwangosi mwenyewe, kwa vurugu na mabmu ya
machozi, na kwanza akapoteza fahamu.
Baada ya kuona hivyo, Addallah Said mwandishi wa gazeti la Tanzania
Daima akamkimbilia RPC ambaye alikuwa katika gari lake la polisi aina ya
Land Cruiser kumuomba awaamuru askari waache kumpiga mwandishi
Daudi Mwangosi.
Wakati huo huo, inaelekea kutokana na kushangazwa na polisi kumpiga
kinyama Daudi Mwangosi, Mkuu wa polisi wa Mafinga OCD Asseri
Mwampamba, aliamua kuingilia , kwanza kwa kuwaamuru na kuwaomba
askari waache kumpiga marehemu Mwangosi.
Mwandisi wa ITV, Renatus Mutabuzi ambaye alirekodi tukio hilo “laivu”
alithibitisha kwa timu ya wachunguzi kuwa licha ya jitihada za OCD Asseri
kuingilia na kumlinda Mwangosi kutokana na kipigo, polisi hao
hawakumsikiliza.
Wakati polisi wakiendelea kumpiga Mwangosi, alijaribu kujiokoa kwa
kumkumbatia OCD Asseri Mwampamba, na baadaye kumwangukia
miguuni mwake kuepuka kipigo zaidi.
Baadhi ya waandishi wa Iringa waliokuwa wamejificha waliweza kupiga
picha za mgando na pia za video za vurugu hizo. Waandishi kutoka Dar es
Salaam waliweza kukusanya habari za vurugu hizo kwa sababu tofauti na
wenzao wa Iringa, polisi hawakuwalenga.
Mwanamke ambaye alijeruhiwa katika vurugu hizo, aliyekuwepo kwenye
eneo hilo la umwangaji damu B alisema kuwa alilala karibu na sehemu
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
18
ambapo Daudi Mwangosi aliuawa ili kuepuka kipigo zaidi kutoka kwa
FFU. Alizungumza na timu ya uchunguzi kwa sharti la kutotajawa.
Mwanamke huyo anadai kuwa aliangalia na hata alimsikia mwandishi
Addallah Said akikikimbilia gari la RPC na kumuomba awaamuru askari
wasiendelea kumpiga Daudi Mwangosi. Alijeruhiwa vibaya na alilazwa
kwenye hospitali ya wilaya ya Mafinga kwa siku tatu.
RPC hakutekeleza ombi la mwandishi huyo. Badala yake alifunga kioo cha
gari lake . Sekunde chache baadaye gari lake lilipiga honi na wakati huo
huo mlipuko wa bomu la machozi ukasikika na kumua mara moja Daudi
Mwangosi.
Kwa sababu marehemu Mwangosi alikuwa bado chini ya miguu ya OCD
Asseri Mwampamba, naye pia alijeruhiwa katika mlipuko huo.
Picha za mgando zinaonyesha polisi akipiga bomu la machozi tumboni
mwa Daudi kwa karibu kabisa.
Kwa masikito makubwa, mwanamke huyo anasema alijua kabisa Daudi
Mwangosi ameuawa mbele ya RPC Michael Kamuhanda.
Kwa Addallah Said na yule mwanamke , kupigwa kwa honi na kutokea
kwa mlipuko kwa wakati mmoja bado ni kitendawili.
Kwa kutoamini kilichotokea, , OCD Asseri Mwampamba alilalama kwa
uchungu kutokana na mlipuko wa bomu la machozi akisema: “Sasa,
umefanya nini ”?
7.6 Taarifa rasmi zinazokinzana
Taarifa rasmi lakini zinazokinzana za polisi kuhusu kuuawa kwa David
Mwangosi zilipatikana kwa vyombo mbalimbali vya habari kuanzia
Septemba 3, 2012. Mamlaka rasmi hazijafuta taarifa hizo mpaka wakati wa
kuchapisha taarifa hii.
Taarifa hizo, vyanzo maalum na vyombo mbalimbali vya habari
vilivyoandika habari hizo vinaorodheshwa kama ifuatavyo:
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
19

20
Taarifa rasmi kwa vyombo vya habari
Taarifa (s)
Mwangosi afariki kutokana na
kitu kizito kilichotupwa na
waandamanaji
• Polisi wakanusha kuhusika
moja kwa moja na kifo cha
mwandishi
• Uchunguzi wa pamoja wa Polisi
na Jeshi utafanywa kutokana na
kifo cha mwandishi.
• Baada ya kuvunjwa kwa ghasia,
Mwangosi anakimbilia walipo
polisi na kitu kama bomu
kikarushwa kundi la watu
wanaokimbia na kumlipua
Mwangosi.
• Watu kadhaa wengine
walijeruhiwa wakiwemo polisi.
• Siko katika nafasi ya
kuzungumza kwa sababu sasa
hivi niko katika chumba cha
maiti cha hospitali ya mkoa ya
Iringa.
• Akanusha kuthibitisha kifo
lakini athibitisha mtu mmoja
amekufa.
• Athibitisha kifo cha mtu mmoja
lakini hana uhakika kama
aliyekufa ni mwandishi wa
Channel Ten
Chanzo
RPC wa Iringa
Michael
Kamuhanda
Kamishna wa
Operesheni wa
Polisi Paul
Chagonja
Taarifa
zimepatikana
kutoka Polisi
makao makuu
RPC wa Iringa
Michael
Kamuhanda
RPC Michael
Kamuhanda
Chombo cha habari /
Tarehe/Toleo Na.
• Kamati ya Kulinda
Waandishi wa Habari
(CPJ).
3/09/2012
Mtandao
• Matangazo ya Channel
Ten, asubuhi ya
Septemba 3, 2012
Reuters
4/09/2012
mtandao
Habari Leo
03/09/2012
02083
1-habari kiongozi Uk. 1
• Matangazo ya Channel
Ten asubuhi ya
Septemba 3, 2012
The Daily News
3/09/2012
10726
Habari kuu
Gazeti la Nipashe
linanukuu Channel Ten
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
21
• RPC anakataa kuzungumza
akisema alikuwa kwenye
mkutano
• Akanusha madai kuwa polisi
wamemuua mwandishi.
• Kilichosababishakifo ni kitu
kilichorushwa na kundi la watu.
Polisi wanachunguza.
• Polisi ilikuwa ikitawanya kundi
la watu. Mwandishi alikuwa
akikimbia kutoka kundi la watu
akifuata polisi. Kitu hicho pia
kilijeruhi watu wengine na
baadhi ya maofisa wa polisi
akiwemo OCS.
• Hawatachukua muda mrefu
kukamiklisha uchunguzi kwa
sababu mashahidi wengi
wanajulikana.
• Mwili wa Mwangosi
umechukuliwa kwa uchunguzi
• Mwandishi aliuawa na bomu la
machozi ambalo halikuwa
limeshughulikiwa vizuri na polisi
• Hatutakuwa katika nafasi ya
kusema nani anahusika na
mauaji hayo timu mbili za
uchunguzi zitakapokamilisha
kazi zake. Hapo ndipo hatua za
kisheria zinapoweza
kuchukuliwa.
Msemaji wa
polisi Advera
Senso
Mkurugenzi
Mkuu wa
Upelelezi DCI
Robert Manumba
Waziri wa
Mambo ya Ndani
Dk. Emmanuel
Nchimbi
(alikariri na
Katibu Mtendaji
wa Baraza la
Habar Tanzanika
(MCT) Kajubi
Mukajanga)
Dk. Emmanuel
Nchimbi –
Waziri wa
Mambo ya Ndani
Gazeti la Nipashe
03/09/2012
03/09/2012
Habari kuu
Gazeti la Mwananchi
03/09/2012
Habari Kuu
The Daily News
04/09/2012
Uk. Wa kwanza habari
ndogo
Habari Leo
04/09/2012
02084
Habari Kuu
Daily News
05/09/2012
10, 728
Habari ya pili kwa
ukubwa (mbele)
7.7 Taarifa rasmi katika muktadha
Kwa upande mmoja Waziri wa Mambo ya Ndani anakiri 4/09/2012
kwamba Daudi Mwangosi aliuawa na bomu la machozi ambalo halikuwa
limeshughulikiwa vizuri, siku inayofuata RPC wa Iringa anatokea kwenye
televisheni akitangaza habari za kuwatupia lawama wafuasi wa Chadema
kwa kutupa kitu kizito kilicholipuka na kumuua Mwanjisi, kujeruhi watu
kadhaa wakiwemo maofisa wa Polisi.
Mashuhuda na mambo kadhaa yaliyochukuliwa kwa video na picha
mgando zinaonyesha kuwa hakukuwa na kundi la watu bali ni wanahabari
na baadhi ya viongozi wa Chadema ambao walikuwa wachache
kulinganisha na idadi ya polisi. Hata hivyo RPC anadai kuwa kuiikuwa na
kundi la watu wakifanya vurugu.
Pia polisi na taarifa zingine rasmi zimeacha kueleza kuwa tukio la
ufunguzi wa tawi lilifanyika katika eneo tulivu A bila ghasia.
Septemba 12, 2012 Konstebo wa Polisi, Cleophase Pasifious Simon (23)
alifikishwa mahakamani kwa akituhumiwa kwa mauaji ya Mwangosi.
.Ushahidi unaonyesha kuwa marehemu Mwangosi alikuwa amezingirwa na
akipigwa na polisi wasiopungua saba. Polisi mmoja akiwa amelenga
bunduki la kupigia bomu la machozi tumboni mwa Mwangosi.
Kukamatwa kwa Konstebo wa polisi na kushitakiwa kunathibitisha Waziri
wa Mambo ya Ndani alichomwambia Katibu Mtendaji wa MCT kuhusu
bomu la machozi “kutokushughulikiwa vizuri” kinyume na jitihada za
kuficha ukweli za RPC wa Iringa, Michael Kamuhanda na maofisa wa polisi
wa makao makuu ya polisi mjini Dar es Salaam.
Cha kushangaza, wakati akihutubia mkutano wa wanahabari uliovunjika
mjini Iringa Septemba 5, 2012 , Mkurugenzi wa Upepelezi wa Makosa ya
Jinai, (DCI), Robert Manumba alisema “matukio ya aina hii yapo na
yataendelea kutokea”. Matamshi haya yalitangazwa sana na vyombo vya
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
22
habari. Manumba alikuwa akijaribu kuwasihi wanahabari wa Iringa ambao
waligomea mkutano aliouitisha mpaka maofisa wote wa polisi wa Iringa
waondoke kwenye ukumbi waliokuwemo. Mgomo huu ulichukuliwa
kufuatia uamuzi wa IPC kugomea kuandika habari za polisi mkoani humo
mpaka uchunguzi kuhusu kuuawa ukamilike Daudi Mwangosi.
8.0 Iliyobaki yote ni historia
Kilichowashangaza waandishi katika hatua hii ni kwamba ghafla polisi
waliwageuka. Hata baada ya kuona kuwa mambo yamekuwa mabaya na
kukimbia kujifisha kwenye vichaka vya karibu, polisi waliwafuata na
kuwalenga kwa mabomu ya machozi huku wakikimbia.
Francis Godwin, mwandishi wa kujitegema, shuhuda na Naibu Katibu
Mkuu wa IPC anakumbuka kuwa polisi wawili walimfukuza mpaka
kwenye vichaka vya kijiji cha Nyololo ambapo alilazimika kuacha gari
lake na kurejea usiku kulifuata.
Wakiwa katika sehemu walipojificha, waandishi walikuwa wakimsaidia
Abdallah Said kuondoa vipande vya nyama ya binadamu vilivyompata
kutoka katika mwili wa Daudi Mwangosi.
Baada ya mkutano wa waandishi wa habari wa asubuhi katika ofisi za RPC,
waandishi waliokuwepo wanakumbuka kuwa askari mmoja mpelelezi
alimfuata Mwangosi na kumwambia : “Ina maana gani kwenda Nyololo
kuandika habari za shughuli za Chadema ambazo zinaweza kuishia na kifo
chako”?
Akiwa anatabasamu, Mwangosi alisema: “ nikifa leo , mwili wangu
hautazikwa ardhini lakini katika mioyo ya watu”. Ilikuwa kama vile
anatabiri kifo chake.
Katibu wa IPC Frank Leonard haelewi kwanini polisi waliwageuka
wandishi wenzake.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
23
“Kila siku saa tano asubuhi , tunashiriki katika mkutano wa waandishi wa
habari unaoitishwa na RPC ofisini kwake. Sisi na maofisa wake tunajua
sana na hata kwa majina. Ni kitendawili kikubwa Polisi
wamewashambulia waandishi wakiwa kazini na hatimaye kumuua Daudi
Mwangosi”.
Katika eneo moja [A], kulikuwa na utulivu ambapo vurugu na umwagaji
damu haukuwepo ambapo katika eneo lingine [B], polisi walitumia nguvu
ya ziada, kupelekea kuuawa kwa Daudi Mwangosi na kujeruhiwa makada
wengine kadhaa wa Chadema.
9.0 Shutuma na kulaaniwa kwa hapa nchini na kimataifa
MCT
Baraza la Habari Tanzania (MCT) limelaani vikali tukio hilo ambalo ni tishio
la moja kwa moja kwa uhuru wa vyombo vya habari. “Hili ni tukio la
kwanza kwa mwandishi wa habari kuuawa akiwa kazini”, Katibu Mtendaji
wa alikaririwa na vyombo vingi vya habari akisema.
MCT inataka mamlaka husika kufanya kila liwezekanlo kuhakikisha kuwa
ukweli wa kilichotokea katika siku ya mauaji hayo ya kikatili unajulikana.
MCT imeshutumu kuwahusisha wanahabari na shughuli za kisiasa na
kumuhusisha na chama cha siasa wakati alikuwa akifanya kazi yake
UTPC
Taarifa ya Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)
umeshutumu vikali mauaji ya Daudi Mwangosi mikononi mwa polisi
wakati akitekeleza kazi zake kama mwandishi wa habari. Taarifa hiyo
imeitaka serikali kuwawajibisha mara moja polisi waliohusika na operesheni
iliyopelekea kifo cha Mwangosi.
UTPC imetaka kufukuzwa kazi mara moja kwa maofisa waliohusika na
kifo marehemu Daudi Mwangosi.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
24
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF)
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limelaani vikali mauaji ya Mwangosi
mikononi mwa polisi.
Katibu Mkuu wa TEF, Neville Meena, anasema hii ni mara ya kwanza
katika historia ya sasa Tanzania kwa mwandishi kuuawa akiwa kazini.
MISA na wengine
Taasisi ya Vyombo vya Habari ya Kusini mwa Afrika (MISA), Kamati ya
Kulinda Waandishi wa Habari (CPJ) na ARTICLE 19, zote zimelaani
kuuawa kwa Daudi Mwangosi akiwa mikononi mwa polisi.
Levi Kabwato, ofisa Programu wa MISA anayeshughulikia Ufuatiliaji wa
Uhuru wa Vyombo vya Habari na Utafiti, alieleza katika taarifa kustushwa
kwake na mauaji ya Mwangosi.
“Hii inastusha. Septemba 2 2012, si siku mbaya kwa uandishi wa habari wa
Tanzania bali kwa eneo zima na dunia yote. Ghasia siyo jibu, hazitatui kitu.
Tunaitaka serikali ya Tanzania kuanzisha uchunguzi na kuwawajibisha wote
waliohusika na upotefu wa maisha,” Kabwato alisema katika taarifa.
CPJ inasema kwamba kifo cha Mwangosi ni cha kwanza kwa mwanahabari
aliye kazini nchini Tanzania tangu taasisi hiyo ilipoanza kuweka rekodi za
kina 1992
ARTICLE 19 imeeleza kusikitishwa na mauaji ya Daudi Mwangosi
mikononi mwa Polisi wa Tanzania, na kuitaka serikali ihakikishe wote
waliohusika wanashitakiwa.
Unesco
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova, pia alishutumu mauaji ya
mwandishi wa habari wa Tanzania, Daudi Mwangosi Septemba2, 2012 na
kuitaka serikali kuchunguza mauaji hayo.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
25
UNESCO inataka serikali ichunguze kifo hicho na kuwashitaki wote
wanaohusika.
Taarifa ya UNESCO inasema: “ Ni muhimu kwa demokrasi na utawala wa
sheria kwamba waandishi waruhusiwe kufanyakazi zao na kutumia haki
yao ya kujieleza kwa usalama.”
10.0 Hitimisho na Mapendekezo
Mauaji ya David Mwangosi mikononi mwa polisi wakati akiwa kazini ni
tishio kwa uhuru wa habari.
Uhuru wa habari ni kumwezesha waandishi kufanyakazi bila vitisho ama
ghasia na waweze kuripoti wakiwa huru bila kudhibitiwa.
Kama mwandishi, Daudi Mwangosi alikuwa akitimiza haki yake ya
kikatiba kufanya “kazi nzuri”.
Kwa vyombo vya habari na hasa waandishi, haijalishi kama Kamanda wa
Mkoa wa Polisi ameipiga marufuku shughuli za Chadema katika kijiji cha
Nyalolo au la.
Ilikuwa ni jambo ka maslahi ya umma kwa vyombo vya habari ambalo
vyombo vya habari vilistahili kuripoti kadri mambo yalivyokuwa
yaakiendelea na watu wenyewe kufanya uamuzi.
Kimsingi, wakati wote na katika matukio yote, mazuri ama mabaya,
waandishi lazima wawepo na wachukuliwe kama watu wasio na upande
wowte.
Pia, Polisi walitumia nguvu ya ziada bila sababu dhidi ya watu wasio na
silaha katika kijiji cha Nyololo village.Katika hatua ya mwisho, ikawa vita ya
polisi dhidi ya waandishi wa habari na hatimaye kuuawa kwa Daudi
Mwangosi.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
26
Timu ya uchunguzi haikubali kabisa suala la kukosea utambulisho wa mtu.
Waandishi wanane waliokuwep katika kijiji cha Nyololo waliweza
kutambulika kwa urahisi, hasa kutokana na mambo kwenda salama katika
eneo la uslamaa [A].
Waandishi walikuwa na Kamera, vidaftari na kalamu na wengine kama sio
wote walikuwa wanafahamika sana na polisi wa Iringa.
Sasa imebainika wazi kwamba Polisi walikuwa wanawawinda waandishi
wa Iringa ambao walikuwa wakiwajua.
Mapambano ya Chadema na Polisi katika Kijiji cha Nyololo habari zake
zilikusanywa na waandishi kutoka Dar es Salaam pia. Kwanini walikuwa
waandishi wa Iringa ndiyo walilengwa katika ghasia hizo.!
Uhasama na chuki iliyokuwepo kati ya RPC wa Iringa na marehemu Daudi
Mwangosi katika kipindi chote cha saa kadhaa tangu mkutano wa
waandishi wa habaria na dakika chache kabla ya mauaji yake mbele ya RPC
huyo huyo katika kijiji cha Nyololo Septemba 2, 2012 unaibua maswali
mengi kuliko majibu.
Waandishi sita wa Iringa wameathirika na msongo wa mawazo kutokana na
kiwango cha ghasia walizofanyiwa na polisi na wanafikiria kuachana na kazi
ya uandishi. Mmoja anapanga kuwa mchungaji kwa kuhofia maisha yake.
Mamlaka husika zahitaji kuwa na mipango ya kuwaelimisha polisi jinsi ya
kushughulika na vyombo vya habari hasa na wandishi wa habari. Lengo liwe
kuboresha mahusiano ya kikao kati ya pande hizo mbili..
Hii inatokana na uhusiano mbaya iliyoibuka kati ya waandishi wa Iringa
na polisi wa mkoa tgangu robo ya mwisho wa 2011. Uhusiano huu kati ya
pande hizi mbili umekua tangu 2011 ambapo aliyekuwa OCD wa Iringa
Mohamed Semunyu alipoamriwa ana bosi wake kulipa kamera ya
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
27
mwandishi aliyoiharibu bila sababu ya maana.
Inashinda ufahamu wa kawaida kwamba matukio mawili ya yanayofanana
katika siku moja ynashughulikiwa tofauti.: Moja linashughulikiwa na
ukatili na nguvu kubwa kwa kuwalenga wanahabari wa Iringa.
Katika tukio la kwanza, RCO aliamua Chadema wanaweza kuendelea na
masuala yao ya ndani katika ofisi yao na katika tukio la pili Mkuu wa polisi
wa mkoa anaamua shughuli hizo zisimamishwe kwa vyovyote na hata kwa
nguvu.
Akigusia kwa kiasi mpambano wa Nyololo kati ya Polisi na wafuasi wa
Chadema, Rais Jakaya Kikwete katika hotba yake ya kila mwezi kwa taifa
kwa mwezi wa September 2012, alisisitiza polisi kuepuka matumizi ya
nguvu za kupita kiasi na kuwakumbusha watanzania na wanasiasa
kuheshimu sheria za nchi na kuiona polisi kama wasimamizi wa amani na
usalama.
Rais alifafanua kuwa Jeshi la Polisi lina mamlaka ya kuruhusu au kuzuia
haki ya kufanya mikutano na maandamano ya vyama vya siasa.
Taarifa za awali za maofisa wa ngazi za juu kuhusu mauaji ya M wangosi
zilitofautiana na mtu anapoziangalia kutokana na ushahidi uliopatikana ni
dhahiri kulikuwa na jitihada za kuficha ukweli.
Tukio hilo limeharibu sifa ya Tanzania kimataifa kama nchi ya amani na ya
demokrasia.
Mauaji ya Mwangosi yalitokea wakati wa kufanyika mkutano wa Chama
cha Umoja wa Mabaraza ya Habari Duniani (WAPC) ambapo MCT ilikuwa
mwenyeji wake.
Katibu Mkuu wa WAPC, Chris Conybeare, alimwambia waziri wa Habari,
Dk. Fenella Mukangara: “Wakati waandisi wanauawa demokrasi pia
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
28
inakufa.. tukio hili moja limeanza kuichafua sifa yaTanzania ya kuendeleza
uhuru wa habari”.
Zaidi ya Polisi saba chini ya uongozi wa RPC Michael Kamuhanda kwa
pamoja wamemzingira na kumpiga Daudi Mwangosi. Kwanini wengine
hawajashitakiwa, si suala linalohitaji uelewa wa kawaida.
Hata hivyo uchunguzi hauwezi kuthibitisha kama mauaji hayo ya
Mwangosi yalipangwa.
Ripoti ya Timu Maalum ya Uchunguzi iliyowasilishwa kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa
kuzingatia Adidu za Rejea ilizopewa na Baraza la Habari Tanzania Septemba 5, 2012.
RIPOTI YA TIMU MAALUM YA UCHUNGUZI ILIYOTEULIWA NA
BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) NA JUKWAA LA WAHARIRI
TANZANIA (TEF) KUCHUNGUZA MAZINGIRA YALIYOPELEKEA KUUAWA
KWA MWANDISHI WA HABARI DAUDI MWANGOSI SEPTEMBA 2, 2012
KATIKA KIJIJI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA
29

30
11.0 Picha za mauaji ya Daudi Mwangosi
Daudi Mwangosi
akiwa mwenye
furaha (kaka
mduara) waka
akimhoji Kamanda
wa Polisi
wa Mkoa wa
Iringa, Michael
Kamuhanda
(kulia) kaka
kijiji cha Nyololo
muda mfupi
kabla ya mauaji
yake.
Askari wa kikosi
cha FFU wakiwa
wamejiandaa
kaka kijiji cha
Nyololo
Polisi wakiwa
wamemzingira
na wakimpiga
vibaya mwandishi
Daudi
Mwangosi.
Aliuawa hapo
hapo.

No comments:

Post a Comment